

Kufuatia kikosi cha klabu ya Yanga kufungwa bao 1-0 na Stand United katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara huko Shinyanga, Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali, ameutaka uongozi kumrejesha haraka Beno Kakolanya.
Akilimali ameibuka tena akieleza ana wasiwasi kama Yanga itafanya vizuri msimu huu kutokana na kipa huyo kuondolewa akiamini ndiye nguzo stahiki katika lango la Yanga.
Mzee huyo ameeleza wasiwasi wake kuwa hana uhakika kama timu itafanikiwa kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu kwa kumtegemea Klaus Kindoki, Ibrahim Hamid na Ramadhan Kabwili kwenye lango.
Ameeleza anamwamini zaidi Kakolanya kuwa ni imara anapokuwa langoni na akisema anashangaa kwanini mpaka sasa hajarejeshwa kikosini.
"Nina wasiwasi na Yanga kuchukua ubingwa msimu huu kwani katika nafasi ya lango mpaka sasa Kakolanya hayupo, nautaka uongozi umrejeshe haraka sana ili atusaidie kufanya vizuri" amesema.
Ikumbukwe Kakolanya aliondolewa na Kocha Mkuu wa timu, Mwinyi Zahera kufuatia kugomea kusafiri na timu kwasababu ya madai ya fedha zake za usajili na mshahara.



0 Comments