Windows

Kundi la Weusi kurudisha bidhaa zao sokoni


Kundi la muziki wa hip hop Bongo la Weusi limeeleza kuwa wanajipanga kwa ajili ya kuingiza
bidhaa zao mpya sokoni baada ya kusimama kwa muda.

Msanii kutoka kwenye kundi hilo, Joh Makini akizungumza na Clouds FM amesema walisimamisha kutoa bidhaa zao kutokana na wizi (kufoji). 

"Tunampango wa kurudi kwenye soko la kuuza nguo na hata kama mnakumbuka sisi tulikuwa wasanii wa kwanza kwanza kufanya biashara ya kuuza tshirt na nguo zingine lakini watu walikuwa wanatoa copy za vitu vyetu na walikuwa wanafanikiwa sababu tulikuwa hatufanyi kwa ukubwa ule," amesema Joh Makini.

Kwa sasa kundi la Weusi linafanya vizuri na wimbo wao mpya unaokwenda kwa jina la Wapoloo baada ya kufanya vizuri na wimbo wao uitwao Swagire.



Post a Comment

0 Comments