Windows

Alichosema RC Makonda baada ya kumuona Askofu Gwajima


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameeleza kuwa yeye na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Josephat Gwajima wanahistoria ndefu zaidi.

RC Makonda ameeleza hayo leo kwenye ukumbi wa mikutano wa JNICC jijini Dar es Salaam ambapo ulifanyiwa mkutano mkuu wa kisekta wa Wizara ya Madini.

"Nimemuona rafiki yangu Gwajima hapa, simama wakuone kidogo, mimi na yeye tuna historia ndefu kidogo kwa hiyo na huku wameshaninoa wengi kuanzia enzi za umoja wa vijana, kwa hiyo mzee hata kama kuna mapambano unaweza ukanituma," amesema RC Makonda.

Utakumbuka uhusiano wa wawili hao ulingia doa mwaka 2017 baada ya RC Makonda kumtaja Askofu Gwajima katika orodha ya watu walioshukia (tuhumiwa) kujihusisha na biashara au kutumia dawa la kulevya.



Post a Comment

0 Comments