Windows

Kocha wa Simba SC atamani kuongeza mshambuliaji wa kimataifa








Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kati wachezaji wa kigeni ambao wanafanya majaribio kwenye kikosi chao, kuna nafasi kubwa ya kumsajili mshabuliaji, Sadney Urikhob kutoka Namibia.

Kocha huyo amesema kuwa anaendelea kumuangalia kila mchezaji kwenye mazoezi ya kikosi hicho lakini anamfikiria zaidi Urithob kwani uwezo.

“Ila nadhani kama tukiamua kumchukua mmoja basi straika Mnamibia anafaa kwani ana kitu ambacho anaweza kukiongeza ndani ya timu yetu na tukaongeza makali hasa kwenye eneo letu la ushambuliaji,” amesema Aussems.

Wachezaji ambao wanafanya majaribi Simba SC ni eki, Lamine Moro, kiungo Jean Bitar Ourega raia wa Ivory Coast pamoja na washambuliaji Hunlede Kissimbo na Urithob.

Post a Comment

0 Comments