KOCHA wa timu ya Biashara United, Amri Said amesema Yanga wasitarajie wepesi kupata matokeo mbele ya kikosi chake kwenye mchezo wao wa kombe la Shirikisho amejipanga kubeba matokeo Uwanja wa Taifa.
Biashara United itacheza na Yanga Uwanja wa Taifa Januari 31 huku timu zote zikiwa zimepoteza michezo yao ya mwisho kwenye mashindano waliyoshiriki, Yanga ilifungwa na KK Sharks mabao 3-2 michuano ya SportPesa Cup na Biashara United ilifungwa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC mchezo wa Ligi Kuu.
Said amesema hana mashaka na uwezo wa wachezaji wake kutokana na maandalizi ambayo anayafanya kikubwa anachofikiria ni kupata ushindi kwenye mchezo wake na anamini dakika 90 zitaamua.
"Yanga wasifikiri ni kazi nyepesi kupata matokeo mbele ya Biashara, mechi yetu kwetu ni zaidi ya fainali ukizingatia ni ya mtaano hivyo ni lazima wachezaji waonyeshe upambanaji kwenye mchezo wetu.
"Nawaheshimu wapinzani wetu ni timu nzuri na ni kubwa ila hilo halitupi mashaka kwani mpira unachezwa Uwanjani, tunawaomba mashabiki watupe sapoti," alisema Said.
0 Comments