

Wakati juzi Simba ikitangaza kumfuta kazi aliyekuwa kocha wake Mkuu Patrick Aussems, kocha wa viungo Adel Zrane naye amerejea kwao akiomba ruhusa ya siku 10 kushughulikia matatizo binafsi
Kuondoka kwa Zrane inaweza kuwa ishara yuko mbioni kuungana na Aussems ambaye inaelezwa huenda akaibukia Afrika Kusini kunako klabu ya Polokwane City
Uongozi wa Simba umepanga kulisuka upya benchi lake la ufundi baada ya kuachana na Aussems
Kocha wa Polisi Tanzania Selemani Matola anatajwa kutua Simba kuchukua nafasi ya kocha msaidizi Denis Kitambi ambaye anakaimu nafasi ya kocha Mkuu
Mchakato wa kumsaka kocha mkuu tayari umeshaanza
Kwa habari zaidi Download App ya soka kiganjani kutoka Play Store.



0 Comments