

Uongozi wa klabu ya Polisi Tanzania umesema unasubiri kukamilika kwa mchakato wa kuvunjwa kwa mkataba ili kumruhusu kocha wao Selemani Matola kujiunga na Simba
Mwenyekiti Msaidizi wa Polisi Tanzania Robert Munisi amesema baada ya uongozi wa Simba kuonyesha nia ya kumtaka Matola, walikutana nao kwa ajili ya majadiliano na kufikia mwafaka
Munisi amesema Simba wanapaswa kuvunja mkataba wa Matola na klabu hiyo kwa kulipa kiasi cha fedha zilizoainishwa kwenye mkataba aliosaini mwezi Julai mwaka huu
"Kimsingi tulishakubaliana kinachosubiriwa ni kukamilishwa mchakato wa kuvunja mkataba ambapo Matola anapaswa kulipa fedha ambazo kulingana na makubaliano ya mkataba aliosaini ni mara tatu ya mshahara ambao anapokea," alisema
Matola anarejea Simba kuwa kocha msaidizi ikielezwa kuwa atachukua nafasi ya Denis Kitambi ambaye kwa sasa anakaimu nafasi ya kocha Mkuu baada ya Patrick Aussems kutimuliwa
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.



0 Comments