

Aliyekuwa kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera leo atakutana na viongozi wa timu hiyo kufuatilia malipo ya madai yake
Zahera aliyetua nchini Jumanne iliyopita, hakupata nafasi ya kuonana na viongozi ambao waliambatana na timu jijini Mwanza kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Alliance Fc
Zahera amesema viongozi walimwambia aandike madai yake yote ili waweze kuyajadili kwenye Mkutano huo
Inaelezwa uongozi wa Yanga umeshamlipa sehemu ya fedha za kuvunja mkataba wake, madai ya sasa ni fedha alizokuwa akitumia kuihudumia timu
Kwenye moja ya mahojiano yake na vyombo vya habari, Zahera alisema ametumia zaidi ya Tsh Milioni 100 kuihudumia klabu ya Yanga
Kwa habari zaidi Download App ya soka kiganjani kutoka Play Store.



0 Comments