Aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera ametoa muda wa wiki moja kwa uongozi wa Yanga kumlipa stahiki zake
Zahera aliyerejea nchini wiki iliyopita ametishia kwenda kushitaki FIFA kama hatakamilishiwa malipo yake
Mcongomani huyo kwa sasa yuko nchini kwa takribani wiki ya pili ambapo ametishia kuwa atapeleka malalamiko FIFA na Yanga italazimika kumlipa hata gharama anazotumia sasa wakati akisubiri kulipwa stahiki zake
Kinachofanywa na Zahera ni kama 'kuikomoa' Yanga baada ya kuvunja mkataba wake mwezi uliopita huku mwenyewe akionekana kutoridhishwa na uamuzi huo
Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amemtaka Zahera kuwa na subira kwani atalipwa
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments