Uongozi wa Yanga umelazimika kuchukua hatua za haraka kufuatia uamuzi wa baadhi ya wachezaji wake kutumia kigezo cha kukosa mishahara kuvunja mikataba
Mmoja wa viongozi amekiri kuwepo kwa changamoto ya kulipa mishahara miezi miwili iliyopita
Hata hivyo amesema wiki ijayo wachezaji watalipwa mishahara ya miezi mitatu
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya Sadney Urikhob kuvunja mkataba huku Lamine Moro nae akichukua uamuzi kama huo
Inaelezwa uongozi wa Yanga uliridhia kuvunja mkataba wa Sadney, lakini suala la Lamine lililoibuka wikiendi hii, litatolewa ufafanuzi siku ya Jumanne
Keshokutwa Jumanne, uongozi wa Yanga huenda ukazungumza kwa kina kuhusu sakata hilo
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments