Windows

Yanga kujipima nje ya jiji



Mashabiki wa Yanga wa nje ya jiji la Dar es salaam wamekuwa na shauku ya kuiona timu yao kwani kwa baadhi ya mikoa wanapata nafasi hiyo mara moja tu huku mikoa mingine ambayo haina timu zinazoshiriki ligi kuu wakiishia kuwaona kupitia runinga

Habari njema wakati huu ambao ligi imesimama, Yanga itafanya ziara mikoani kucheza mechi za kirafiki ambazo zitakuwa sehemu ya maandalizi ya mchezo wa kombe la FA dhidi ya Iringa United na ule wa watani wa jadi dhidi ya Simba

Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema baada ya wachezaji kurejea kutoka mapumziko, wataweka hadharani ratiba ya program nzima ya maandalizi

Baada ya mchezo dhidi ya KMC, wachezaji walipewa mapumziko ya siku mbili na wanatarajiwa kurejea mazoezini kesho Alhamisi

Wakazi wa mikoa ambayo haina timu zinazoshiriki ligi kuu kama Dodoma, Kigoma, Rukwa na kwingineko huenda wakapata nafasi ya kutembelewa na mabingwa hao wa kihistoria

Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store

Post a Comment

0 Comments