Miongoni mwa mapendekezo yaliyotolewa jana na viongozi wa Matawi kwenye Mkutano na Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla, ni kuharakishwa kwa mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji
Awali Dk Msolla alitangaza kuwa mchakato huo ungeanza mwezi May 2020
Lakini baada ya mapendekezo ya viongozi wa matawi, mchakato huo sasa umependekezwa uanze mwezi March 2020
Uongozi wa Yanga umeahidi kuwashirikisha wanachama wake katika kila hatua ili suala hilo liwe limekamilika kabla ya kuanza msimu ujao
Masuala mengine yaliyojadiriwa kwenye mkutano huo ni pamoja na usajili wa dirisha dogo lililofunguliwa leo
Ikiwa tayari Yanga imekamilisha usajili wa mshambuliaji mmoja (Tarik Seif) , washambuliaji wengine wawili watasajiliwa
Washambuliaji hao mmoja mzawa na mwingine wa kigeni
Ditram Nchimbi ndiye mchezaji mzawa anayetajwa kuwa mbioni kusajiliwa baada ya Yanga kufikia makubaliano na Azam Fc ambapo mchezaji huyo ataigharim Yanga Tsh Milioni 20
Lakini pia maboresho ya safu ya ulinzi hasa upande wa kushoto yatafanyika
Mapema leo baada ya GSM kufanikiwa kumrejesha beki Lamine Moro aliyekuwa amevunja mkataba wake kutokana na madai ya mishahara, wadhamini hao wa Yanga walibainisha kuwa watasimamia zoezi la usajili wa dirisha dogo
Michakato tayari inaendelea na pengine wiki hii Wanajangwani watarajie kuwafahamu nyota zaidi waliosajiliwa
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments