Kocha Mkuu wa Simba Sven Van Der Broeck jana alianza rasmi majukumu ya kukinoa kikosi cha mabingwa hao wa soka Tanzania Bara
Van Derboroek aliyetambulishwa mapema wiki iliyopita, hakuanza majukumu yake mara moja kutokana na kutokamilika kwa vibali vyake vya kazi
Hata hivyo Vanderbroeck alikuwa akihudhuria mazoezi yaliyokuwa yakisimamiwa na kocha Selemani Matola
Ujio wa makocha hao wapya umeibua vita mpya ya namba miongoni mwa wachezaji wa Simba
Mapema baada ya kutambulishwa kuwa kocha msaidizi wa Simba, Matola alizungumza na wachezaji ambapo aliwataka wasahau zama za kocha Patrick Aussems
"Tunajua kocha aliyepita alikuwa na taratibu zake, nasi tumekuja na taratibu zetu. Tumeanza mazoezi leo kila mchezaji anapaswa kuonyesha uwezo"
"Uwezo wako wa uwanjani ndio utakupa nafasi kwenye kikosi cha kwanza. Hatutaangalia majina, watakaofanya vizuri mazoezini ndio watacheza," aliongeza Matola
Kauli hiyo ni kama imeamsha mzuka wa wachezaji kwani mazoezi ya timu hiyo yamekuwa kama mechi
Kila mchezaji akijituma kuhakikisha anawashawishi mabosi hao wa benchi la ufundi
Ni kawaida mabadiliko ya benchi la ufundi huja na neema kwa baadhi ya wachezaji ambao pengine walikuwa hawapati nafasi kwenye kikosi cha kwanza, huanza kucheza
Kwa habari zaidi Download App ya soka kiganjani kutoka Play Store
0 Comments