Kampuni ya GSM imefanikiwa kumrejesha beki kisiki Lamine Moro na leo uongozi wa Yanga pamoja na Lamine akiwa na Meneja wake wamethibitisha kuwa sintofahamu iliyojitokeza imemalizika
Lamine amerejea kutumikia mkataba wake wa miaka miwili na klabu ya Yanga
Mkurugenzi wa GSM Tanzania Mhandisi Hersi Said amesema wamemrejesha Lamine kwa kuwa wanafahamu ni mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Yanga
Aidha amesema kurejea kwa beki huyo kisiki ni mwanzo tu, baada ya kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili, watashirikiana na uongozi wa Yanga kukiboresha kikosi cha timu hiyo
"Lamine ana mkataba na Yanga, lakini wote tunajua kuna mambo yalitokea mpaka akaondoka, sisi GSM tumehakikisha mambo yote yanarudi kuwa sawa. Huu ni mwanzo tu kuna wachezaji watakuja hatutaki kuzungumza sana ila mambo yakiwa sawa wakisha saini mikataba tutawaweka wazi," amesema
Ushirikiano huu wa GSM na Yanga ni dalili njema kuelekea mchakato wa mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store
0 Comments