Windows

Mkwasa atamba, furaha inarejea jangwani



Kocha wa muda wa Yanga, Boniface Mkwasa ameridhishwa na jinsi ya wachezaji wake wanavyocheza kwa maelewano kitu ambacho ni kizuri amewataka mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kukaa mkao wa kula.

Mkwasa anakimu nafasi hiyo baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mkongomani Mwinyi Zahera kutupiwa virago mwanzoni mwa mwezi uliopita.

Kocha huyo wazamani wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' amesema kadri siku zinavyozidi kwenda ndipo kikosi chake kinavyo imarika na wanatarajia kufanya vizuri katika mechi zinazo fuata.

"Viwango vya wachezaji vinaimarika siku hadi siku ni jambo zuri, wachezaji wana morali na wanapokea vizuri mafunzo tunayo wapa, tunatajia kufanya vizuri kwenye ligi na michuano ya FA iliyo mbele yetu," alisema Mkwasa.

Yanga inarejea leo jijiji Dar es Salaam kutoka mkoani Kigoma ilipokuwa na mechi mbili za kifariki dhidi ya Mwangungo FC walioshinda 2-1 na Kigoma Stars ambao waliibuka na ushindi wa mabao 3-0.



Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.

Post a Comment

0 Comments