Disemba 22 2019 kikosi cha Simba kitashuka uwanja wa Uhuru kuikabili Arusha Fc ukiwa ni mchezo wa kombe la FA (ASFC) raundi ya tatu
Kuelekea mchezo huo ambao utakuwa wa kwanza kwa kocha mpya wa Simba Sven Vanderbroeck, Mbelgiji huyo tayari ameanza majukumu ya kuwanoa mabingwa hao wa nchi huku akifanya mabadiliko kadhaa katika program zake za mazoezi
Vanderbroeck ameongeza muda wa mazoezi ambapo sasa wachezaji watafanya mazoezi mara mbili kwa siku
Wakati wa Patrick Aussems timu ilifanya mazoezi mara moja tu kwa siku na mara chache kufanya mara mbili kutegemea na ratiba ya mechi zinazowakabili
Jana Vanderbroeck aliisimamia timu yake ikifanya mazoezi mara mbili, asubuhi na jioni
Aidha kocha huyo pia ametaka mazoezi yafanyike pasipo kushuhudiwa na mashabiki wala waandishi wa habari
Mbelgiji huyo amesema mashabiki na waandishi wa habari wataruhusiwa kushuhudia mazoezi hayo ya mabingwa wa nchi katika siku maalum lakini sio kila siku
Amesisitiza kuwa si vyema kila mtu kushuhudia mazoezi hasa wanapokuwa wanafanya mazoezi ya kimbinu, ni rahisi kwa wapinzani wao kubaini kile wanachokifanya
Hataki masihara
Katika siku zake chache na kikosi cha Simba, Vanderbroeck ameonyesha ni kocha asiyependa masihara
Ameonyesha kuwa na msimamo na wakati mwingine kuwa mkali pale anapoona wachezaji hawafanyi vile anavyowaelekeza
Kwa ujumla ameanza vyemal, uwepo wa kocha mzawa Selemani Matola pia unamsaidia kutimiza majukumu yake kwa urahisi
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments