Windows

Usajili dirisha dogo kusubiri mapendekezo ya Sven




Uongozi wa Simba haujaonyesha kuwa na papara badala yake wamempa nafasi ya kocha wao mpya Sven Vandenbroeck kuangalia wachezaji wake na kisha atoe kauli juu ya usajili.

Afisa Mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Senzo Mazingisa amesema kwamba licha ya dirisha la usajili kufunguliwa, hawawezi kusajili bila kuangalia matakwa ya benchi la ufundi.

"Tunamuacha kocha na benchi lake aangalie kikosi kilichopo ili ajue kama kuna mabadiliko ambayo yatahijika, hatuwezi kusajili mchezaji kama kocha hajasema"

Licha ya kwamba Senzo amempa rungu Sven kwenye usajili, bajeti ya Simba kwenye dirisha dogo kupitia mkutano mkuu ilitangazwa kuwa ni Sh 76 Milioni 76, ambapo imeelezwa kwamba wataangalia mapendekezo ya kocha kama yataendana na bajeti yao.

"Kila kitu kitaendana na matakwa ya kocha, tutajua mchezaji yupi na atatoka wapi kulingana na bajeti tuliyonayo," alisema

Post a Comment

0 Comments