Windows

Wanachama waridhia uwanja kuitwa Simba Mo Arena




Wanachama wa klabu ya Simba wameridhia uuwanja wa Bunju kuitwa Simba Mo Arena

Mo ndiye aliyegharamia awamu yote ya kwanza ya ujenzi wa uwanja huo, hivyo Wanachama wamemtunuku heshima hiyo

Mapema akizungumza kwenye Mkutano huo wa Wanachama, Mo alisema awamu ya pili ya Ujenzi itawashirikisha Wanachama na mashabiki

"Jana tumeshawaonyesha uwanja wetu wa mazoezi ambapo kutakuwa na viwanja vizuri na vya kisasa, cha nyasi bandia na majani asilia, pamoja na viwanja hivyo tumejenga chumba cha kubadilishia nguo chenye ubora na fensi ya kulizunguka eneo la viwanja."

"Hii ni awamu ya kwanza, yanayokuja pale Bunju Complex yatafurahisha nchi na Wanasimba wote, katika suala la miundombinu ya Bunju niwahakikishie wanachama wenzangu mambo yatakuwa bul bul"

"Awamu ya pili ya ujenzi wa Bunju Complex, kujenga hosteli yenye vyumba vya kulala, gym, ofisi za benchi la ufundi, jiko na kantini ya chakula, nutritional center, chumba maalum cha kitaalam kwa uchambuzi wa mechi zetu na mazoezi, pamoja na technical room."

"Mradi huu unatarajiwa kuwa na thamani ya Tsh. Bilioni 2.5 na kwa kuanzia kama mwanachama na Mwenyekiti wa Bodi nitachangia kiasi cha Tsh. milioni 500. Wanasimba wanahamu yakuchangia ujenzi na upanuzi wa Bunju Complex."

"Kiasi kilichobaki tutafanya fundrising ili kupata fedha inayotakiwa, bila shaka tutafanikiwa ili kwenye msimu wa 2021/22 tuwe kwenye hostel zetu. Kazi yangu ni kuhakikisha wachezaji wanapata mazingira bora na mishahara mizuri ili waweze kufocus na kushinda"



Kwa habari zaidi Download App yaSOKA KIGANJANI kutoka Play Store.

Post a Comment

0 Comments