Windows

Wanachama Simba kupendekeza jina la Uwanja Bunju



Klabu ya Simba inatarajiwa kufanya mkutano mkuu wa mwaka kesho Jumapili ambapo wanachama wamepewa nafasi ya kupendekeza jina la uwanja wao uliopo Bunju B nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Hayo yamesema na Msemaji wa klabu hiyo Haji Manara wakati wa kuwaonyesha wanachama wao maendeleo ya uwanja wao ambao utaanza kutumika kwa ajili ya mazoezi na Januari mwakani utazinduliwa rasmi

"Kwenye mkutano ndiko kutapendekezwa jina la uwanja huu kwamba utaitwaje hivyo tusubiri hiyo kesho (Jumapili), hii ndiyo Simba inayowajali wanachama wake," amesema Manara

Simba imejenga viwanja viwili Bunju ambapo kimoja ni cha nyasi bandia kingine nyasi za kawaida ambapo sasa timu yao itaanza kufanya mazoezi na kupunguza gaharama za kulipia viwanja vya mazoezi ambapo sasa hutumia uwanja wa Gymkhana.

Mbali na uwanja wa Gymkhana pia walikuwa wanatumia uwanja wa Boko Veterani ambapo viwanja vyote ni vya kukodi.



Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.

Post a Comment

0 Comments