Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Senzo Mazingisa amesema kwa sasa hawafikirii mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Yanga ambao utapigwa Januari 04 2020
Akizungumza kwenye hafla maalum ya utambulisho wa uwanja wa klabu ya Simba iliyofanyika Bunju mapema leo, Senzo alisema wanajipanga kwa mechi ya FA hatua ya 64 bora
Simba itacheza mchezo huo wa FA dhidi Arusha FC katika uwanja wa Taifa, Disemba 23
Senzo amesema kwa sasa wanajipanga ili kuhakikisha wanashinda mchezo dhidi ya Arusha na kuvuka hatua ya 32 bora
"Kabla ya Yanga tunatakiwa kucheza FA na Arusha FC kwahiyo baada ya mchezo huu ndio tunaweza kuwazungumzia Yanga. Kila kitu kina muda wake," alisema Senzo.
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments