Windows

Van Der Broeck Mbelgiji anayehusishwa kuchukua nafasi ya Aussems



Wakati Wanamsimbazi wakisubiri taarifa rasmi ya viongozi wao kuhusu kocha mpya, kocha wa zamani wa timu ya Taifa ya Zambia Sven Van Der Broeck anatajwa kuwa yuko nchini akihusishwa na nafasi hiyo

Kocha huyo kijana inaelezwa kuwa huenda ndiye atakayetangazwa kuwa mkufunzi wa Simba

Van Der Broeck raia wa Ubelgiji hana jina kubwa sana lakini ni kocha anayeonekana kuyakimbilia mafanikio kwa kasi kubwa

Kwani katika umri mdogo (miaka 40) tayari amepata nafasi ya kuaminiwa kupewa majukumu ya kufundisha timu za Taifa

Simba jana ilimtangaza Selemani Matola kuwa kocha msaidizi huku kukiwa na taarifa kuwa kocha mkuu huenda akatangazwa leo

Je ni Van Der Broeck au Chambeshi? tusubiri..



Kwa habari zaidi Download App ya Mwana Msimbazi kutoka Play Store

Post a Comment

0 Comments