Windows

Umemsikia Nugaz? usajili wa kutikisa nchi unakuja



Pamoja na kutawala vyombo vya habari wiki yote iliyopita kwa bandika-bandua ya usajili, uongozi wa klabu ya Yanga umesema bado haujamaliza

Mpaka sasa Yanga imesajili nyota wanne ambao ni Tariq Seif Kiakala, Haruna Niyonzima, Ditram Nchimbi na Adeyum Saleh

Pia mabingwa hao wa kihistoria wako kwenye majadiliano ya kumsajili mshambuliaji Yikpe Gnamien raia wa Ivory Coast

Yikpe yuko nchini tangu juzi akisubiri kukamilika kwa michakato ya ndani kabla ya kupewa mkataba

Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amesema usajili wa funga kazi bado haujafanyika

"Kuna usajili mkubwa utafanyika karibuni, hatujamaliza bado. Kabla dirisha halijafungwa tutashusha usajili wa kutingisha Dar es salaam na hata ukanda wa Afrika Mashariki," ametamba Nugaz

"Sijajua, tunaweza kutua Misri, tunaweza kutua Morocco au Afrika Kusini..tukikwama basi tutatua Msumbiji lakini tukikwama kabisaa basi tutaibukia DR Congo ambako tutarudi na mshambuliaji mmoja hodari wa kutia magoli.."

"Tumewapa mashabiki nafasi ya kuchagiza usajili huo kwani tunaamini nao wana nafasi yao"

"Lakini wakati huohuo tunawataka mashabiki wakae tayari kwa mabadiliko.. wakae tayari kwa mfumo mpya wa usajili wa kadi za wanachama na mashabiki.. andaeni shilingi elfu moja kwa muda wa miezi miwili ili ukiwa na elfu 60 uweze kupata mambo yote mazuri yanayokuja"

Post a Comment

0 Comments