Windows

Simba 'yamchomoa' Matola Kilimanjaro Stars




Uongozi wa klabu ya Simba umewasiliana na Shirikisho la soka Tanzania (TFF) ili kupata ruhusa ya kumchukua kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania bara 'Kilimanjaro Heroes' Suleiman Matola kuanza kibarua cha kuwanoa mabingwa hao wa nchi

Matola yupo kwenye kambi ya Kilimanjaro Heroes inayojiandaa na michuano ya Cecafa itakayo fanyika nchini Uganda kuanzia Disemba 07

Taarifa inasema Matola anakamilisha taratibu zote na atajiunga na kikosi cha Simba mda wowote kuanzia Jumanne

Inaelezwa TFF imeridhia maombi hayo ya klabu ya Simba ambapo nafasi ya Matola kwenye kikosi cha Kili Stars itachukuliwa na Zuberi Katwila.

Simba iliachana na Patrick Aussems mwishoni mwa wiki huku moja ya sababu ikiwa ni kushindwa kusimamia nidhamu ya wachezaji

Kwa sasa Simba inanolewa na kocha Msaidizi Denis Kitambi ambaye naye ataondoka



Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.

Post a Comment

0 Comments