Windows

Senzo aahidi Simba ya kisasa



Ile kauli ya 'Simba Next Level' haikubuniwa kwa ajili ya kufurahisha mashabiki tu, bali inafanyika kwa vitendo ili kuitofautisha klabu hiyo na zingine hapa nchini.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingiza amesisitiza kuwa Simba itaendeshwa na kufanya mambo yake kisasa hasa baada ya kuwaingiza wanachama wake kwenye mfumo maalumu wa kadi za kielektroniki.

Akizungumza leo Jumamosi wakati wa kuzindua rasmi kadi hizo kwa kushirikiana na Benki ya Equity, Senzo alisema Simba inastahili kuwa kwenye mfumo huo kutokana na ukubwa wa jina la klabu hiyo Afrika.

"Leo ni siku muhimu sana kwa Simba kwani, tunaweka historia ya kuingia katika mfumo wa kadi za kisasa kwa wanachama, inastahili mabadiliko haya kwa kuwa, ni klabu kubwa inayotakiwa kuendeshwa kisasa zaidi Afrika.

Pia, Senzo alitumia fursa hiyo kumpongeza aliyekuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crecentius Magori ambaye mfumo huo ulibuniwa chini yake na kuanza kufanyiwa mchakato wakati wa uongozi wake.

"Kadi hizi zina faida kubwa kwa mwanachama ikiwemo kuzitumia katika kufanya manunuzi kwenye maduka makubwa tena kwa punguzo la bei.

"Pia, mishahara ya wafanyakazi na wachezaji wa Simba itakuwa ikifanyika kupitia benki ya Equity ambayo kwa sasa ni mshirika wetu wa karibu na ndio wamehusika na kuandaa kadi hizi za kisasa," amesema Senzo.


Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.

Post a Comment

0 Comments