Windows

Simba Queens yaichapa Yanga Princess 3-1




Simba Queens imeendeleza ubabe dhidi ya watani zao Yanga Princess baada ya kuwachapa mabao 3-1 kwenye mchezo wa ligi kuu ya Wanawake uliopigwa uwanja wa Karume

Mabao ya Mwanahamisi Omary na Neema Kilinga aliyefunga mabao mawili, yameihakikishia Simba Queens ushindi ambao unawafanya wafikishe alama 10 baada ya kushuka dimbani mara nne

Hicho ni kipigo cha tatu mfululizo Simba Queens iliwazawadia watani zao Yanga Princess

Aidha kipigo hicho cha Yanga Princess ni salama tosha kwa kaka zao kuelekea mchezo wa ligi kuu utakaopigwa Janury 04 2020



Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.

Post a Comment

0 Comments