Baada ya kuwaondoa Kocha Mkuu Patrick Aussems na kocha msaidizi Denis Kitambi, uongozi wa klabu ya Simba huenda ukaachana na mtaalam wa misuli Mjerumani Paul Gomez
Gomez alijiunga na Simba mwezi Julai mwaka huu wakati timu hiyo ikiwa Afrika Kusini kwenye maandalizi ya msimu mpya
Hata hivyo mtaalam huyo anadaiwa kutokuwa na ufanisi hasa linapokuja suala la huduma kwa wachezaji majeruhi
Majeruhi yaliyomuweka nje nahodha John Bocco yanaweza kuwa moja ya sababu zitakazomuondoa Simba
Kabla ya kupelekwa Afrika Kusini kufanyiwa uchunguzi wa kina, kwa nyakati tofauti Bocco alirejea kikosini na baadae kuondolewa baada ya kubainika hajapona sawasawa
Uongozi wa Simba umepanga kulisuka upya benchi lote la ufundi ambapo mabadiliko mengine yanaweza kumkumba kocha wa makipa Mharami Mohammed
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store
0 Comments