Aliyekuwa kocha msaidizi wa Polisi Tanzania Selemani Matola, kuanzia leo Alhamisi, Disemba 05 2019 sio mwajiriwa wa timu hiyo baada ya makubaliano ya kuvunja mkataba wake kufikiwa
Uongozi wa klabu ya Polisi Tanzania, umethibitisha kuwa umevunja mkataba na Matola baada ya pande zote mbili kuridhiana
"Uongozi wa Polisi Tanzania umeridhia ombi la Mwalimu Seleman Matola la kuvunja mkataba wake na Klabu yetu kuanzia leo tarehe 05/12/2019," imesema taarifa ya Polisi Tanzania
"Tunamshukuru kwa mchango wake katika kipindi chote alichohudumu katika Klabu yetu"
Baada ya hatua hiyo kufikiwa ni dhahiri sasa wakati wowote klabu ya Simba itatamtangaza Matola kuwa kocha wake msaidizi
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store
0 Comments