Windows

Makocha 108 waomba kazi Simba



Afisa Habari wa Simba Haji Manara amesema makocha 108 wamejitokeza kuomba kazi ya ukufunzi wa klabu ya Simba

Simba iko katika mchakato wa kusaka kocha mpya baada ya kuachana na aliyekuwa kocha wao Mkuu Patrick Aussems

Akizungumza mapema leo kwenye mahojiano na redio Wasafi FM akiwa ameongozana na Mkurugenzi wa Wanachama Hashimu Mbaga, amesema idadi hiyo ya makocha wamejitokeza mpaka sasa huku wakiendelea kupokea maombi

Ashangazwa na kauli za Aussems

Juzi wakati anaondoka nchini baada ya kumalizana na uongozi wa Simba, Aussems alidai hakuwa huru katika utendaji kazi wake ambapo allitupia lawama Bodi ya Wakurugenzi kuwa iliingilia majukumu yake huku akidai hakushirikishwa kwenye usajili

Manara ameeleza kushangazwa na kauli za kocha huyo ambazo amezitoa baada ya kuwa amefutwa kazi

"Kulingana na umri wake na uzoefu wake nimeshangaa kuona Aussems akiikashifu bodi ambayo ndio ilimuajiri."

"Bodi haina sababu ya kumpiga majungu Aussems, Bodi iwe inampiga majungu kwani kawachukulia wake zao," alisema Manara.

Akizungumzia suala kuondolewa kwa kocha huyo Manara alisema ni jambo la kawaida kwa timu kuachana na kocha kwani hilo limekuwa likitokea sehemu yoyote ile.

"Simba na Azam zote zimefukuza makocha, Azam imefundishwa na makocha wawili ndani ya mwaka mmoja, lakini mbona kawaida maana nao ni timu tajiri," alisema Manara.

Aponda mbinu za Aussems ugenini

Manara amedai pamoja na mafanikio waliyopata kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu uliopita, timu ilikuwa dhaifu ilipocheza ugenini

"Rekodi ya kufungwa mabao mengi nje ya nchi katuletea Aussems, kabla ya hapo hatukuwa hivi. Ni kwa sababu ya mbinu zake kutobadilika awapo nyumbani na ugenini. Unacheza na Al Ahly kwao unapangaje washambuliaji wawili?," alihoji Manara


Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJI kutoka Play Store.

Post a Comment

0 Comments