Beki Lamine Moro amevunja mkataba wake na Yanga baada ya timu hiyo kushindwa kumlipa mshahara kwa miezi mitatu
Ameungana na Sadney Urikhob ambaye pia amevunja mkataba wake kutokana na tatizo kama hilo
Mapema mwaka huu, nyota hawa walikuja Simba kufanya majaribio wakisaka nafasi ya kusajiliwa
Hata hivyo Patrick Aussems aliyekuwa kocha wa Simba hakuridhiswa na viwango vyao
Wakati Sadney akionekana ni yuleyule, Lamine ameonyesha utofauti katika kipindi kifupi alichocheza Yanga
Raia huyo wa Ghana ndiye aliyekuwa beki wao bora akitengeneza pacha na Kelvin Yondani
Baada ya kuvunja mkataba na Yanga, tetesi zimemuhusisha kutua Msimbazi dirisha dogo
Miongoni mwa nafasi ambazo huenda zikaongezwa nguvu, safu ya ulinzi inaweza kuwa
Dirisha dogo la usajili linafunguliwa wiki ijayo, tusubiri...
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments