Mshambuliaji wa Yanga Sadney Urihob amewaaga mashabiki baada ya kuitumikia timu hiyo kwa takribani miezi sita tu
Sadney ameondoka Yanga baada ya makubaliano ya kuvunja mkataba baina yake na uongozi wa timu hiyo
"Ilikuwa heshima kwangu kuvaa jezi ya njano na kijani, naushukuru uongozi wa Yanga pamoja na mashabiki, nawatakia kila la kheri," Sadney ameandika kwenye ukurasa wa mtandao wa Instagram
Ni dhahiri suala la Sadnye kuondoka Yanga sio tetesi tena, mabosi wa Yanga wana nafasi ya kufanya usajili wa mshambuliaji mwengine wa kigeni
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments