Baadhi ya wachezaji wa Yanga wametumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kumuaga mshambuliaji Sadney Urikhob ambaye amevunja mkataba wake na mabingwa hao wa kihistoria
Mlinda lango Farouk Shikalo amemuaga pro huyo akimtakia maisha mema huko anakoelekea
"Kila la kheri kaka, tunakutakia maisha mema huko uendako," aliandika Shikhalo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Uongozi wa Yanga uliridhia kuvunja mkataba wa nyota huyo baada ya yeye mwenyewe kuomba
Mabingwa hao wa kihistoria wataitumia nafasi yake kufanya usajili mwingine
Kuna taarifa kuwa Yanga huenda itaachana na nyota wengine wa kigeni
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments