Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema hadi kufikia mwezi May 2020 Yanga itakuwa imebadili mfumo wake wa uendeshaji kutoka wa sasa (mfumo wa wanachama) kuwa mfumo wa hisa
Dk Msolla aliyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu changamoto mbalimbali zinazoikabili timu hiyo
"Nawapa ahadi wanachama, ifikapo mwezi Mei 2020 tutabadili mfumo wa klabu kuwa wa uwekezaji. Tukishirikiana vyema na wanachama tutalifanikisha hili katika muda huo"
Mapema Dk Msolla alibainisha changamoto za kiuchumi zinazoikabili Yanga huku akitaja timu hiyo kuwa na madeni yanayozidi Tsh Bilioni mbili huku mapato yakiwa hayatoshi
Yanga inakabiliwa na malimbikizo ya madeni ya mishahara ya wachezaji na makocha hadi miaka mitatu nyuma
Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji ndio hitaji la wengi wanaoamini Yanga itaweza kusimama kiuchumia
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments