Windows

Molinga hakuomba kuvunja mkataba



Mshambuliaji David Molinga sio miongoni mwa walioandika barua ya kuvunja mikataba yao na Yanga kama ilvyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari

Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema mchezaji huyo aliomba ruhusa kwenda Ufaransa kumuuguza mwanawe

Molinga jana alifika Makao Makuu ya klabu kuomba ruhusu na wakati huo akifuatilia VISA

Dk Msolla amesema kama VISA haitapatikana kwa haraka Molinga ameahidi kuendelea na mazoezi na wachezaji wengine ambao wamerejea kujifua jana baada ya mapumziko ya siku tano

Yanga imethibitisha ni Sadney Urikhob na Lamine Moro pekee ambao waliandika barua ya kuvunja mikataba yao

Sadney ameruhusuwa kuondoka baada ya uongozi kutokuwa na mpango nae lakini Lamine bado anahitajika ambapo Dk Msolla amesema watamshawishi mchezaji huyo aendelee kubaki huku akiahidi kulipa madai yake yote leo sambamba na wachezaji wengine


Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.

Post a Comment

0 Comments