Windows

Marcelo alianza vizuri, akapotea



Yanga inatarajiwa kufanya usajili wa beki wa kushoto dirisha dogo litakapofunguliwa Disemba 16 ili kumaliza changamoto katika nafasi hiyo

Wakati wa Zahera, Mcongomani huyo alilazimika kumtumia Ally Mtoni 'Sonso' baada ya Muharami Issa 'Marcelo' kushindwa kuonyesha makali

Mkwasa nae hajamtumia kabisa Marcelo, ni dhahiri beki huyo ameshindwa kumshawishi

Katika mechi zote tano (nne ligi, moja ya kirafiki), Mkwasa amemtumia kiungo Jaffar Mohammed upande wa beki wa kushoto

Marcelo alisajiliwa na Yanga akitokea klabu ya Singida United ambayo ilikuwa imemsajili kutoka Malindi Fc

Usajili wake ulikamilishwa baada Gadiel Michael kukataa kusaini mkataba mpya zikiwa zimebaki siku chache kabla ya dirisha la usajili kufungwa

Rais wa Singida United Mwigulu Nchemba aliidhinisha Marcelo atue Yanga ikiwa ni ahadi aliyotoa katika hafla ya kuichangia Yanga iliyofahamika kama KUBWA KULIKO

Alipata nafasi kucheza mechi kadhaa za kirafiki ukiwemo mchezo wa wiki ya Mwananchi dhidi ya Kariobangi Sharks ya Kenya

Mchezo pekee wa kimashindano aliocheza ulikuwa dhidi ya Township Rollers akicheza kwa dakika 45 tu

Tangu wakati huo Marcelo hajaonekana katika mchezo wowote wa Yanga. Huenda atatolewa kwa mkopo dirisha dogo



Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.

Post a Comment

0 Comments