Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
Klabu ya Yanga imetuma maafisa wake wa Kamati ya Ufundi kwenda nchini Rwanda kushuhudia mchezo wa ligi kati ya AS Kigali dhidi ya Gicumbi siku ya Jumapili lengo likiwa kumuangalia kiungo Haruna Niyonzima
Yanga imedhamiria kumrejesha Niyonzima 'nyumbani' dirisha dogo lakini wametaka kujiridhisha na uwezo wake kabla ya kumpa mkataba
Awali Yanga ilipanga kutumia michuano ya CECAFA Challenge inayoanza keshokutwa nchini Uganda kumuangalia kiungo huyo
Hata hivyo Rwanda ilijitoa kwenye michuano hiyo
Kufuatia changamoto zilizojitokeza kutokana na usajili uliopita, Yanga haitaki kurudia makosa ya kusajili nyota ambao wana uwezo wa kawaida
Pamoja na kuwa Niyonzima amecheza hapa nchini lakini hakuna anayefahamu maendeleo yake katika kipindi cha miezi sita, hivyo ni suala la kujiridhisha nae kabla ya kumpa mkataba
Yanga pia inahusishwa kumuwania beki wa kushoto wa Rayon Sports Erick Rutanga, maafisa hao pia huenda wakakamilisha dili la nyota huyo
Mabingwa hao wa kihistoria wamepania kuboresha kikosi chao mapema na pengine kuwatumia baadhi ya wachezaji wapya kwenye mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa January 04 2020
Baadhi ya nyota wapya ambao watatua Yanga dirisha dogo huenda wakaanza kuonekana mapema kwenye mazoezi
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments