

Kocha wa zamani wa Gor Mahia na AFC Leopards Zdravko Logarusic amehusishwa na Simba SC kumrithi Patrick Aussems
Mabingwa hao wa nchi wanasaka kocha mpya baada ya kuachana na Aussems mwishoni mwa wiki
Logarusic aliyewahi kufundisha Simba, alikuwa kocha wa timu ya Taifa ya Sudan kabla ya timu hiyo kuachana nae baada ya mkataba wake kumalizika
Pamoja nae, makocha wengine wanaotajwa pia yumo Mfaransa Didier Gomes
Gomez aliwahi kuinoa Rayon Sport ya Rwanda pamoja na Cotton Sport ya Cameroon aliyoisaidia kutinga nusu fainali ya michuano ya kombe la shirikisho barani afrika
Wengine ni Pierre Lechantre ambaye ndiye aliyemuachia Aussems, Florent Ibenge ambaye kwa sasa anainoa AS Vita
Hata hivyo uwezekano wa kumpata Ibenge wakati huu ni mdogo kwani kocha huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya DR Congo anaiongoza AS Vita ambayo iko hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Kwa habari zaidi Download App ya soka kiganjani kutoka Play Store.



0 Comments