Michuano ya CECAFA Challenge Cup inaanza leo nchini Uganda lakini timu za Taifa za Tanzania Bara 'Kili Stars' na ndugu zao wa Zanzibar Heroes wao watashuka dimbani kesho Jumapili
Kili Stars itaanza kampeni ya michuano hiyo kwa kuumana na Kenya katika mchezo utakaopigwa saa kumi jioni Jumapili wakati mapema saa saba na nusu siku hiyohiyo Zanzibar Heroes itaumana na Sudan
Wachezaji wa Kili Stars wameapa kuwa iwe isiwe lazima wapambane ili waweze kupata ushindi wa kwanza kwenye michuano hiyo dhidi ya Kenya
Kili Stars inahitaji kushinda angalau mechi mbili ili kujihakikishia nafasi ya kuingia nusu fainali kwani kila kundi timu mbili zitakazoshika nafasi za juu zitaingia nusu fainali
Nyota wa Kili Stars Juma Abdul na Bakari Mwamnyeto wamesema wamejipanga vema kupeperusha bendera ya taifa wana imani ya kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo
"Tupo tayari kwa ajili ya kupambana na kupata matokeo chanya tunatambua kwamba ushindani ni mkubwa hilo halitupi shida kwa kuwa tumejiandaa kushinda mashabiki watupe sapoti pamoja na dua," alisema Mwamnyeto baada ya mazoezi ya kwanza yaliyofanyika jijini Kampala jana
Kwa upande wake Abdul alisema: "Tumejipanga vema na tumefanya maandalizi kiujumla, kila mchezaji anahitaji kuona timu inashinda, mchezo wa mpira ni ushindani tunawaheshimu wapinzani wetu tunajua kwamba nao wamejipanga kama sisi hivyo hatutawadharau"
Kilimanjaro Stars imepangwa kundi B pamoja na timu za Kenya, Sudan na Zanzibar
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments