Kocha Mkuu wa Manchester City Pep Guardiola amesema kuwa mshambuliaji wa Manchester United, Marcus Rashford na Anthony Martial walikuwa na moto mkali jambo lililofanya wakapoteana mapema.
City ilikubali kichapo cha mabao 2-1 mbele ya Manchester United na kuifanya iwe nyuma ya vinara Liverpool kwa tofauti ya pointi 14.
Guardiola amesema kuwa pamoja na kupoteza jumla mchezo huo hawezi kukubali kuwaachia ubingwa kirahisi.
"Tulipoteza mbele ya Manchester United kutokana na ubora wa Rashford na Martial hawa walikuwa mwiba mkali mwanzo mwisho.
"Lakini haijalishi hata kama tungekuwa nyuma kwa pointi 10,14 au 25 lazima tuendelee kupambana kwa nguvu kubwa hadi mwisho," amesema.
City imejikusanyia jumla ya pointi 32 kwenye Ligi Kuu England huku vinara wakiwa na pointi 32 wote wamecheza mechi 16.
0 Comments