Baada ya kuwasili kutoka mkoani Kigoma, kikosi cha Yanga kitaendelea na mazoezi kwenye uwanja wa Uhuru kujiandaa na mchezo wa kombe la Azam (ASFC) dhidi ya iringa United
Mchezo huo utapigwa siku ya Jumamosi, Disemba 21 katika uwanja huo
Mabingwa hao wa kihistoria watakabiliwa na wiki ngumu ya kufunga mwaka 2019 kwani watashuka dimbani mara nne
Baada ya mchezo dhidi ya Iringa United, Yanga itaelekea mkoani Mbeya ambako Disemba 24 itacheza na Mbeya City dimba la Sokoine
Disemba 27 itarudi Sokoine kupepetana na Tanzania Prisons
Watafunga mwaka Disemba 30 kwenye uwanja wa Uhuru kwa kuumana na Biashara United
0 Comments