Windows

Adeyum atambulishwa Yanga




Yanga imetambulisha usajili wa mlinzi wa kushoto Adeyum Saleh aliyetua kutoka klabu ya JKT Tanzania

Adeyum amesaini kandarasi ya miaka miwili kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria

Akizungumza katika hafla ya utambulisho wake uliofanyika Makao Makuu ya klabu ya Yanga, Afisa Mhamasishaji Antonio Nugaz amesema usajili wa Adeyum ni mapendekezo ya Kaimu Kocha Mkuu Charles Mkwasa

"Tulikuwa na majina manne mezani katika nafasi ya beki wa kushoto. Kocha Mkwasa akampendekeza Adeyum kuwa ndiye aina ya mchezaji ambaye anahitajika Yanga kwa sasa," amesema

Aidha Nugaz amesema zoezi la utambulisho wa nyota wapya litaendelea siku ya kesho Alhamisi, Ijumaa na watafunga kazi kwa usajili wa kishindo Jumanne ijayo



Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.

Post a Comment

0 Comments