Simba imetangaza bajeti ya Sh6.1 bilioni kwa msimu huu 2019/2020 katika kuhakikisha klabu hiyo itatetea ubingwa wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kurudi katika Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Bajeti hiyo ilitajwa kwenye mkutano mkuu wa klabu ya Simba uliofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere.
Katika bajeti hiyo, klabu ya Simba imetenga Sh76.8 Milioni za usajili wa dirisha dogo utakaoanza hivi karibuni.
Mbali na usajili wa dirisha dogo, klabu ya Simba itatumia Sh 4.16 Bilioni kwa ajili ya mishahara ya wachezaji na Sh 408 kwa ajili ya bonusi.
Katika bajeti hivyo, vyanzo vya mapato vitaiingizia klabu ya Simba Sh 5.814 Bilioni ambayo ni pungufu ya Sh373 milioni katika mapato ya klabu.
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments