Wakati klabu ya Simba ikitarajiwa kumtangaza kocha wake mpya wiki hii, Mkufunzi wa Nkana Fc Beston Chambeshi ameachia ngazi kuinoa klabu hiyo
Chambeshi ni miongoni mwa makocha ambao walikuja nchini kufanyiwa usaili na Simba inayosaka mrithi wa Patrick Aussems
Hata hivyo, kulingana na taarifa iliyoripotiwa na vyombo vya habari nchini Zambia mapema leo, Chambeshi ameomba kujiuzulu kuinoa Nkana ili apate muda wa kupumzika kabla ya kufahamu mustakabali wake
Pamoja na kudaiwa kuwa tayari ameshasaini mkataba Simba, wakati akiwaaga wachezaji wa Nkana kwenye mazoezi ya jana, Chambeshi aliwaambia kuwa bado hajasaini kwenye timu yoyote
Chambeshi ni miongoni mwa makocha wenye mafanikio makubwa nchini Zambia, akipata mafanikio zaidi wakati akizifundisha timu za taifa za vijana
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store
0 Comments