Windows

Simba kujifua Gym kwa siku tatu



Kocha Msaidizi wa Simba, Denis Kitambi ameamua kuhamishia mazoezi kwa siku tatu Gym baada ya kufanya mazoezi ya uwanjani kwa siku kadhaa

Kitambi alikuwa akifanya mazoezi mbalimbali kwa maana ya nguvu, mbinu na mengineyo ambayo yote walikuwa wakifanya uwanjani.

Baada ya mazoezi jana, Kitambi anayeiongoza Simba wakati huu ambao kocha Mkuu Patrick Aussems amesimamishwa, alisema leo Jumamosi hawatafanya mazoezi ya uwanjani bali watakwenda kufanya mazoezi ya Gym

"Tutafanya mazoezi ya Gym zilizopo Golden Tulip Tower ili kuweka miili sawa ya wachezaji kwani walitumika zaidi uwanjani," amesema


Aidha kutokana na timu kutokuwa na ratiba ya mechi ya ligi hadi mwakani, kumekuwa na shauku kwa mashabiki kuiona timu yao ikipata mechi za kirafiki

Kitambi amesema suala hilo litaamuliwa na uongozi wa Simba lakini mpaka sasa bado hajapewa maelekezo ya mchezo wowote wa kirafiki

"Ambalo lipo mbele yangu kwa wakati huu ni kuandaa timu kuwa fiti na hali ya ushindani lakini kuhusu kucheza mechi za kirafiki hili bado sijaambiwa na uongozi"

Post a Comment

0 Comments