

Pamoja na mkanganyiko wa ratiba, kikosi cha Simba kinatarajiwa kuendelea na mazoezi kesho Jumanne baada ya mapumziko ya siku mbili
Mabingwa hao wa Tanzania Bara hawaonekani kuwa na mchezo hadi January 04 2020 watakapo-wakabili watani zao Yanga katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Taifa
Baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting juzi, wachezaji walipewa mapumziko hayo
Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema benchi la ufundi litaandaa program maalum ya mazoezi wakati wote ambao ligi itakuwa imesimama kupisha michuano ya CECAFA Chalenji inayoanza Disemba 07 nchini Uganda
Ligi hiyo inaendelea kwa mechi tatu kpigwa katika viwanja mbalimbali;



0 Comments