

Timu ya Taifa ya Wanawake ya Kenya imeibuka mabingwa wa michuano ya CECAFA mwaka 2019 wakiwapokonya Tanzania Bara tonge mdomoni kwa kushinda mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi
Mabao yote ya Kenya yalifungwa na mshambuliaji wao hatari Mwanadada Jentrix Shikangwa
Kenya ni kama imelipa kisasi kwa Tanzania Bara kwani mwaka 2016 michuano hiyo ilipofanyika Kenya, timu hizo zilikutana kwenye fainali na Kilimajaro Queens kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kushinda taji hilo
Pamoja na kutawala mchezo Kilimanjaro Queens walishindwa kutumia nafasi walizotengeneza huku Kenya wakitumia vyema nafasi zao kujipatia mabao hayo moja likifungwa kwa mkwaju wa penati



0 Comments