Viungo watatu wa Yanga Abdulaziz Makame, Feisal Salum na Mohammed Issa 'Banka' wataukosa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Alliance Fc hapo kesho Ijumaa
Wachezaji hao wako kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Zanzibar ambayo imeanza maandalizi ya michuano ya CECAFA Challenge inayoanza Disemba 07 nchini Uganda
Uongozi wa Yanga umesema baada ya mchezo dhidi ya JKT Tanzania, wachezaji hao walipewa ruhusa kwenda kujiunga na kambi ya Zanzibar Heroes
Hata hivyo baadae Bodi ya Ligi ikawataarifu kuwa wanapaswa kucheza mechi zao mbili za viporo dhidi ya Alliance Fc na KMC
Hivyo nyota hao pia wataukosa mchezo dhidi ya KMC ambao huenda ukapigwa Disemba 02 uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam
Kaimu kocha Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amesema pamoja na kuwakosa nyota hao, wana matumaini watafanya vizuri katika michezo yote miwili
Baadhi ya mashabiki wameonyesha kukerwa kwa uongozi wa Yanga kukubali kucheza mechi hizo bila ya wachezaji hao
Pengine viongozi wangeweza kuchukua hatua ya kuwarudisha kikosini hasa kwa mchezo dhidi ya KMC ambao utapigwa jijini Dar es salaam
Michezo hii ya viporo ina uhumuhimu mkubwa kwa Yanga kushinda hasa ikizingatiwa wanawafukuzia watani zao Simba ambao wapo kileleni mwa msimamo wa ligi
Kama Yanga itashinda mechi zote za viporo itafikisha alama 25 na kuwa sawa na Simba
Kufungwa au hata sare ni matokeo ambayo yataivurugia Yanga hesabu
Ni wakati ambao Yanga inapaswa kumtumia kila mchezaji ambaye yuko fiti ili kupata ushindi
0 Comments