Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Senzo Mazingisa amewatoa hofu mashabiki wa timu kuwa nahodha wa timu hiyo John Bocco atapona na kurejea akiwa imara baada ya matibabu yake nchini Afrika
Juzi uongozi wa klabu ya Simba ulitangaza kumpeleka Bocco Afrika Kusini kufanyiwa uchunguzi zaidi wa jeraha la misuli linalomsumbua
Bocco anatibiwa katika Hospitali ya Netcare Rosebank iliyopo jijini Johannesburg
Senzo amesema Rosebank ni sehemu salama, ana matumaini makubwa kuwa Bocco atapata tiba nzuri na kurejea nchini kuendelea na majukumu yake
0 Comments