Windows

Tulihitaji matokeo ya ushindi - Mwandila



Kocha Msaidizi wa Yanga Noel Mwandila amesema baada ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya Ruvu Shooting na kulazimishwa sare ya mabao 3-3 dhidi ya Polisi Tanzania, mchezo wa leo dhidi ya Coastal Union walihitaji kushinda jambo ambalo wamelifanikisha

Akizungumza baada ya mchezo, Mwandila amewapongeza wachezaji kwa kujituma muda wote wa mchezo tofauti na mechi iliyopita

"Nawapongeza wachezaji kwa kufanikiwa kushinda leo. Tulihitaji matokeo haya hasa baada ya kuanza msimu vibaya"

"Kwa ujumla wachezaji wamepambana kupata ushindi huu. Mchezo uliopita hatukucheza vizuri baada ya kufunga bao, kisha tukaruhusu mabao matatu"

"Leo nawapongeza wachezaji kwa kufanikiwa kutoruhusu bao"

Nae kiungo Abdulaziz Makame ambaye alifunga bao pekee la Yanga kwenye mchezo huo, amesema anajisikia faraja kwa kuipatia Yanga ushindi muhimu

"Najisikia kama nimetua mzigo. Yanga wamenipokea vizuri, kutopata ushindi kwenye mechi zilizopita ni matokeo yaliyokuwa yakituumiza sana wachezaji"

"Leo tumeshinda, ni jukumu letu hivyo nafurahi nimetimiza wajibu wangu kama mchezaji wa Yanga"a

Post a Comment

0 Comments