Windows

Ligi Kuu yasimama kupisha kalenda ya FIFA



Baada ya mechi ya leo kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union ambayo mwamuzi aliwazawadia Yanga bao, ligi imesimama kupisha kalenda ya michuano ya FIFA na CAF

Ligi itaendelea Oktoba 23 ambapo mabingwa watetezi Simba wataendeleza burudani kwa mashabiki wao watakapoikabili Azam Fc inayoshika nafasi ya pili

Simba na Azam ndio timu pekee ambazo zimeshinda michezo yao yote

Simba imeshuka dimbani mara nne, imeshinda mechi zote na ina alama 12

Azam Fc imeshuka dimbani mara tatu na imeshinda mechi zote pia

Mpaka sasa Simba ndio wababe wa ligi kwa wingi wa pointi na mabao

Post a Comment

0 Comments