


KAMPUNI ya Michezo ya kubashiri SportPesa kwa kushirikiana na Kampuni ya mtandao wa simu Tigo Tanzania wamechezesha droo ya kuwapata washindi wa wiki ya tano wa simu janja aina ya Samsung A10s huku ikiwakabidhi washindi wanne wa wiki iliyopita kutoka Dar es Salaam.
Promosheni ya Faidika na Jero imezinduliwa rasmi Septemba 20, mwaka huu ambapo SportPesa kwa kushirikiana na Tigo waliahidi kuwazawadia wateja wake simu janja mpya aina ya Samsung A10s kwa siku 40 na gari mpya aina ya Renault Kwid mpya.

Akizungumza mara baada ya droo ya wiki ya tano Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi SportPesa Tanzania, Tarimba Abbas alisema “Promosheni bado inaendelea ambapo wiki ijayo tunatarajia kuwapa washindi watakaomaliza promosheni na mshindi wa gari mmoja.

“Mpaka sasa tumepata washindi kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Dar, Pwani, Dodoma, Iringa, Morogoro, Mbeya, Lindi, Tunduma pamoja na Zanzibar.”
“Ningependa kuwahamasisha Watanzania kushiriki kwenye promosheni hii kwa hali na mali na kucheza kwa bidii ili waweze kujishindia zawadi zilizopo, vilevile SportPesa tunatoa nafasi kwa Watanzania kubadilisha maisha yao maana zawadi ya gari si kitu kidogo”

“Kupitia huduma zetu kama Jackpot ambayo kwa sasa iko zaidi ya Sh Milioni 250 baada ya kubashiri mechi 13 kwa usahihi zinaweza kumuinua Mtanzania kiuchumi, ubashiri wa kawaida kupitia masoko mbalimbali unaweza kumuinua Mtanzania wa kawaida na kumuwezesha kushinda fedha kila siku.
“Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza washindi wa wiki hii ambao ni Sadick Mihambo, Shazili Sambi (DSM), Mussa Hassan (Mbeya), Chawedi Saidi (Lindi), Mwate Mohammed (Morogoro) na Regan Yusto (Zanzibar),”alisema Tarimba.
The post Mshindi wa Gari jipya la SportPesa kupatikana wiki ijayo appeared first on Global Publishers.



0 Comments